Chamberlain atakuwa kulipa ahadi yake kwa Robertson
Beki wa kushoto wa Liverpool Andy Robertson amefichua kuwa,kuelekea kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu, mchezaji mwenzake Alex Oxlade Chamberlain alimwambia kuwa ataweka jezi yake kwenye frame nyumbani kwake kama atakuwa na assist 10 katika ligi kuu msimu huu.
Beki huyo wa kushoto ijumaa iliyopita kwenye ushindi wa 5-0 dhidi ya Huddersfield alitengeneza magoli mawili na kufikisha Assist 11 katika ligi kuu msimu huu na hivyo kutimiza ahadi yake na AOC.
Chamberlain alikiri awali kuwa ataweka kwenye frame jezi iliyosainiwa ya Robertson nyumbani kwake kando na jezi ya Lionel Messi kama mchezaji huyo wa Scotland atafikisha assist 10 katika ligi kuu msimu huu.
Chamberlain ambaye amerudi uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa siku 367 akiuguza majeraha, sasa ni muda wa kutimiza ahadi yake aliyoweka kwa Robertson.