Pogba ni tatizo kuwa Old Trafford, asema Keane
Nyota wa zamani wa Manchester United Roy Keane amefunguka kuwa kiungo Paul Pogba ni tatizo kubwa katika kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer.
Licha ya Pogba kuomba msamaha baada ya kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa Everton wiki jana, Keane akiongea kuelekea mechi ya Manchester Derby jana kupitia kituo cha Sky Sports amesema kuwa hawezi kuamini maneno ya mchezaji huyo kwani hafikirii kama alimaanisha alichokisema.
.
‘( Pogba) ni kijana mwenye kipaji. Lakini tunaongea kitu kimoja tena na tena. Ni mara nyingi tumemuona katika mechi akiwa hakimbii au kurudi nyuma. Ni tatizo kubwa kwa United’ alisema Roy ambaye ameichezea United kuanzia mwaka 1993 hadi 2005.