Ndanda waingia katika faini kwa kuiga vitendo vya Yanga
Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ( kamati ya masaa 72) imeitoza Klabu ya Ndanda SC faini ya Tsh. 1,500,000 (milioni moja na nusu) kwa kosa la kuingia Uwanjani kwa Kutumia Mlango usio rasmi katika mechi iliyochezwa April 4 mwaka huu dhidi ya Yanga Afrika SC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Hilo ni kosa la kwanza msimu huu kwa timu ya Ndanda kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi wakati Yanga wakiwa wamefanya kosa hilo mara nne msimu huu
Adhabu dhidi ya Ndanda pia ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Taratibu za Mchezo Tanzania.