Newcastle United ni timu isiyobadilika
Ligi Kuu ya nchini England inaelekea ukingoni lakini vita ya Ubingwa kati ya Manchester City na Liverpool inazidi kupamba moto na ngumu kutabiri timu ipi itaibuka kuwa binfwa, tukiachana na hayo klabu ya Newcastle ambayo inashabikiwa na Rais mstaafu wa Tanzania DR Jakaya Mrisho Kikwete bado haina mabadiliko.
Newcastle United ya msimu wa 2017/2018 na Newcastle United ya msimu huu 2018/2019 hazina tofauti yoyote, kama hufahamu Newcastle United iliyochini ya kocha wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez hadi sasa inatakwimu sawa na msimu uliopita kwa kila kitu.
Msimu wa 2017/2018 Newcastle United hadi kufikia michezo yake 35 ilikuwa imeshinda michezo 11, sare michezo 8, imepoteza 16, magoli ya kufunga 35 na kufungwa 44, takwimu hizo zinafanana kila kitu na msimu wa 2018/2019 wakiwa wamecheza michezo 35 pia, kimsingi ni kama timu haijabadilika haijapanda kiwango wala kushuka hadi sasa.