Wallace Karia ni Rais asiyekurupuka
Kwa upande wa soka la Bongo kwa sasa Tanzania habari kubwa na inayoumiza mashabiki wengi wa soka ni kuhusiana na habari ya timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys kuondolewa kwa aibu katika michuano ya AFCON U-17, huku wao ndio wakiwa wenyeji.
.
Serengeti Boys iliyokuwa Kundi A na timu za Uganda, Angola na Nigeria imeondolewa mapema katika michuano hiyo kwa kufungwa katika michezo yao yote mitatu ya makundi.
.
Baada ya kuondolewa katika michuano hiyo baadhi ya wadau na mashabiki wa soka wamekuwa wakishinikiza kocha wa timu hiyo Oscar Mirambo atimuliwe kitu ambacho kimemfikia Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Wallace Karia.
“Kiwango chetu kilikuwa ni kibovu mno kwa hiyo tunasubiria taarifa ya benchi la ufundi ili tuweze kujua ni kitu gani, baada ya ripoti ndio tunaweza tukatoa maamuzi mengine lakini sasa hivi (Oscar Mirambo) bado ni kocha wa Serengeti Boys, bahati mbaya jamani mimi ni Rais ambaye huwa sikurupuki, hao watu walisema nimfukuze Amunike hao hao sasa hivi wanamsifia Amunike, wanambeba Amunike” Wallace Karia akiongea hayo kupitia TBC 1