Wachezaji wa PSG wachangisha pesa za Notre-Dame
Mabingwa wa Ufaransa PSG jana katika katika mchezo wa Ligue 1 ambao waliibuka na ushindi wa nyumbani wa goli 3-1 dhidi ya Monaco, walishuka dimbani wakiwa na jezi za kipekee wakionesha kuguswa kwao na kuungua kwa jengo la Notre Dame Cathedral ambalo ni historia kubwa kwa mji wa Paris na Ufaransa kwa ujumla, PSG wamevaa hivyo kama sehemu ya kuhamasisha na kuchangia pesa za ukarabati wa Notre Dame Cathedral.
Jezi walizokuwa wamevaa wachezaji hao zina picha ya jengo la Notre Dame likiwa kabla ya kushika moto.
Jengo hilo ambalo liliungua na moto wiki iliyopita April 15 liliwanyong’onyesha watu wa Taifa lote na wageni ambao wamewahi kutembelea, wazimamoto zaidi ya 400 walifika katika tukio kupambana na moto huo.
Jezi hizo walizovaa wachezaji wa PSG zikiwa na picha za jengo hilo, mgongoni mwao hayakuandikwa majina yao, na badala yake liliandikwa jina la ‘Notre-Dame’
.
Baadaye PSG wakatangaza kuwa jezi hizo maalum ambazo zilitengenezwa 1000 zitauzwa kwa euro 100( Tsh Laki mbili na elfu 60) kila moja na pesa hizo zitaelekezwa katika mchango wa ukarabati wa jengo hilo.
Hata Monaco nao katika mechi hiyo walivaa jezi maalum ambazo mbele zina-sura ya jengo hilo.