Karia atoa kauli kuhusu tuhuma za rushwa zinazomkabili
Pamoja na kuwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kupitia kwa katibu Mkuu wake Wilfred Kidao kumtetea na kumsafisha Rais wa shirikisho hilo Wallace Karia katika tuhuma za mgao wa rushwa wa Tsh milioni 46 kutoka kwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF), majibu ya TFF na Karia yanatofautiana.
TFF imeeleza na kutoa mchanganuo kuwa pesa alizopokea Rais wa TFF Wallace Karia ni kwa ajili ya miradi ya shirikisho hiyo na ilifanya kazi husika ila Wallace Karia alipohojiwa na TBC1 kwa njia hya simu alikanusha taarifa hizo za kusema tuhuma zilizotajwa hazijataja jina lake zaidi ya kueleza kuwa ni Tanzania FA President “Kwanza kwenye mitandao ile ambayo inatrend haijataja jina langu imesema Tanzania FA President lakini watu wa mitandao ya Tanzania ndio wamebadilisha wameweka jina langu, kipindi hicho Ahmad anaingia katika uchaguzi mimi sikuwa Rais, kwa sababu ukisoma ule mtandao unasema kuwa yule Rais wa shirikisho hakupata hiyo hela , ukisoma ile ya nje sasa. Sisi hapa tunajua maadui ni wengi” alisema Wallace Karia kupitia TBC 1 .
.
Tukukumbushe tu Rais wa CAF Ahmad Ahmad na baadhi ya viongozi wengine wa mashirikisho ya soka Afrika, wameingia katika kashfa ya ubadhilifu wa fedha za CAF, Ahmad Ahmad anadaiwa kuwa aliisababishia CAF hasara ya Tsh Bilioni 2 kwa kuagiza vifaa kupitia kampuni ya Ufaransa ya Tactical Steel.