Son atoa msaada wa Milioni 300 nchini kwao
Staa wa Tottenham Heung Min-Son ametoa msaada wa Pauni 100,000 (Tsh Milioni 300) kwa wahanga wa mlipuko wa moto uliotokea hivi karibuni nchini kwao Korea kusini na kusababisha uharibu wa nyumba takribani 400 huku watu wawili wakithibitika kufariki dunia.
Moto huo ulikatiza eneo la milima kaskazini-mashariki mpaka karibu na mipaka ya Korea Kaskazini.
Mamlaka wamesema hii moja ya janga kubwa la moto kuwahi kutokea katika historia ya Korea kusini.
Wachunguzi wameeleza kuwa moto huo wanaamini ulitokana na cheche za transformer zilizotokea jioni ya April 05. .
“Ninaamini pesa si tatizo. Kitu cha muhimu zaidi ni nia ya kufanya kitu fulani kwa ajili ya wahanga”