Simba na Yanga kuipisha michuano ya AFCON
Mechi za Ligi kuu zitakazochezwa kesho katika Viwanja Viwili tofauti kuchezwa saa 8.00 mchana ili kutoa nafasi kwa watanzania waweze kuangalia michuano ya Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.
Mechi hizo ni Simba SC atakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Yanga atakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Katika michuano hiyo ya AFCON chini ya miaka 17 kesho April 17 zitachezwa mechi mbili, Nigeria dhidi ya Angola na Uganda dhidi ya wenyeji Tanzania.