Zizou asema pengo la Ronaldo halizibiki Bernabeu
Majira ya kiangazi mwaka jana klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ilikubali kumuachia nyota wake wa kimataifa wa Ureno na mshindi wa tuzo tano za mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo na kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia. .
Real Madrid pamoja na kuchukua taji la klabu Bingwa Ulaya mara tatu mfululizo, iliyumba kiasi cha kuamua kumrudisha tena kocha wake wa zamani Zinedine Zidane aliyefanikisha zoezi la kutwaa mataji hayo ya Ulaya mara tatu mfululizo. .
Zidane baada ya kurudi imeelezwa kuwa anaunda upya kikosi chake cha Real Madrid, hivyo mwisho wa msimu huu tutegemee kuona wakiuzwa wachezaji wengi na kununuliwa wengi, ila kocha huyo amekiri Ronaldo aliyedumu na timu hiyo kwa miaka tisa hakuna mbadala wake. .
“Tunaweza kusajili wachezaji wapya lakini hakuna kati yao anayeweza kufanya kilichokuwa kinafanywa na Cristiano Ronaldo, nina uhakika na hili ila hivyo ndivyo maisha yalivyo” alisema Zidane kupitia ESPN UK