Simba waanza kulisaka kombe lao
Baada ya kurejea Jijini Dar es Salaam kutokea Lubumbashi walikokuwa na mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika na kutolewa katika michuano hiyo kwa kufungwa bao 4-1 na TP Mazembe, kikosi cha Simba SC kimeanza safari leo asubuhi kuelekea mkoani Tanga kwaajili ya mchezo wake wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union.
Mchezo huo utachezwa April 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mpaka sasa Simba wana viporo 11 katika ligi kuu msimu huu, wakiwa nafasi ya tatu na pointi 57.