Kocha akiri kipa wake changamoto
Baada ya kupoteza mchezo wa jana wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 dhidi ya Nigeria kwa kufungwa goli 5-4,Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya vijana ‘Serengeti boys’ Oscar Mirambo amekiri kuwa katika nafasi ya Golikipa kuna changamoto katika kikosi chake.
.
” Changamoto kweli ipo kwa Golikipa lakini tunapompa nafasi tena anazidi kuimarika na kujua kuwa alikosea wapi katika mchezo uliopita ” Mirambo
Mirambo aliongeza kuwa japo wamepoteza mchezo wa jana lakini bado Serengeti boys ina nafasi ya kufanya vizuri kwa michezo miwili iliyobaki.
.
Pia alisisitiza kuwa muda huu sio wa kuwalaumu vijana kwa kutofanya vizuri , sasa ni wakati wa kuwaweka sawa ili waweze kufanya vizuri katika michezo iliyobaki.
.
“Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuweza kuwaweka sawa watoto ili wasahau yaliyopita na kujiandaa na mechi zilizobaki” Mirambo
.
Tanzania atakuwa Mgeni wa Uganda katika mchezo unaofuata utakaochezwa April 17 mwaka huu saa 11.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa na mechi ya mwisho watacheza na Angola April 20.