Morocco yajitolewa kumtibu kipa wa Guinea
Moja kati ya habari ya kusikitisha iliyohitimisha michezo ya makundi ya klabu Bingwa Afrika ni tukio lililotokea wakati wa mchezo wa marudiano Horoya AC ya Guinea dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco ambapo mchezo huo marudiano ulichezwa nchini Morocco. .
Tukio la mlinda mlango wa Horoya AC Khadim N’daye ambaye alivunjika mguu wake wa kulia dakika ya 84 alipokuwa akijitahidi kuokoa goli na kujikuta akigongana na mchezaji wa timu yake na kupelekea kuvunjika mguu.
.
Tukio hilo linadaiwa kuwa linaweza kumaliza maisha ya soka ya Khadim au kumuweka nje uwanja kwa muda mrefu.
Pamoja na hayo shirikisho la soka Morocco limetangaza kumsaidia gharama za matibabu yake.
Hata hivyo Khadim amepatiwa matibabu ya awali nchini Morocco. .
Mchezo huo ulimalizika kwa Wydad kupata ushindi mnono wa mabao 5-0, yaliowapeleka moja kwa moja kucheza hatua ya nusu fainali kutokana na mchezo wao wa kwanza ugenini walitoka 0-0, hivyo Wydad anaungana na timu za TP Mazembe, Esperance na Mamelodi katika hatua ya nusu fainali.