Lewandowski na Coman warushiana ngumi mazoezini
Wachezaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski na Kingsley Coman wameripotiwa kupigana jana alhamisi mazoezini na kuamuliwa na wachezaji wenzao.
Kwa mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani, wachezaji hao walitenganishwa na Jerome Boateng na Niklas Sule.
Bild wameripoti kuwa ugomvi huo ulitokana na Lewandowski kuongea maneno ambayo yalimkasirisha Coman.
Wachezaji hao walirushiana maneno kabla ya kurushiana ngumi,kila mmoja akitaka kuipata sura ya mwenzake.
Kocha wa Bayern Niko Kovac awali alitaka kuwapeleka wote katika vyumba vya kubadilishia nguo lakini akabadili maamuzi na kuwaacha wote waendelee na mazoezi kitendo kilichowashangaza wachezaji wengine.
Mwaka jana Lewandowski na Mats Hummels waliliripotiwa kutenganishwa baada ya kugombana mazoezini.
Mke wa Robert Lewandowski,Anna Lewandowska aliwahi kushinda medali ya shaba katika kombe la Dunia la Karate mwaka 2009.