Costa amaliza msimu kwa staili yake
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa amefungiwa mechi nane na shirikisho la soka la Hispania kwa kosa kumtukana mwamuzi Jesus Gil katika kipigo cha 2-0 kutoka kwa Barcelona Jumamosi iliyopita.
Kifungo hicho ina-maana Mhispania huyo atakosa mechi kipindi chote cha msimu kilichobaki kwani Atletico Madrid wamebakisha mechi saba katika LaLiga msimu huu.
Costa amefungiwa mechi nne kwa kumtukania mwamuzi huyo mama yake na mechi nne zingine kuishika mikono ya mwamuzi akimzuia asimuoneshe kadi.