Karuma awapigia debe Twiga Stars
Baada ya Timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ kutolewa katika kuwania mbio za kufuzu michuano ya Olimpoki 2020 Mwenyekiti wa chama cha Soka cha Wanawake Tanzania Amina Karuma amewataka watanzania kuendelea kuiunga mkono timu hiyo.
Twiga Stars ilitolewa na timu ya Wanawake ya Congo April 9 mwaka huu kwa kufungwa kwa goli 1-0 nchini Congo huku mchezo wa awali uliochezwa nchini Tanzania April 5 mwaka huu walitoka sare ya bao 2-2.
Karuma amesema anaiamini Twiga stars maana ni timu nzuri na imefanya vizuri katika michuano mbalimbali,ikiwemo kuwa Bingwa wa Jumuiya ya Africa Mashariki mwaka jana,baada ya kushinda katika michezo yake iliyochezwa nchini Burundi.
” Niwaombe watanzania waendelee kuiunga mkono timu yangu ya Twiga Stars maana ni timu nzuri inawachezaji wanaojua nini wafanye sema haikuwa bahati yetu kuweza kufanya pata ushindi katika mchezo wetu na Congo pale kwao lakini wachezaji walijituma sana” Karuma