Wawa kuwakosa TP Mazembe
Beki wa kati wa Klabu ya Simba Pascal Wawa atawakosa TP Mazembe kwenye mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika utakaochezwa April 13 mwaka huu Lubumbashi nchini Congo kutokana na kuwa majeruhi.
Wawa alipata maumivu kwenye misuli ya paja katika mchezo wa awali uliowakutanisha Simba na Tp Mazembe April 6 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lmchezo ukiisha kwa sare ya bila kufungana.
#Worldsports14 imezungumza na Meneja wa Klabu ya Simba Patrick Rweyemamu kutaka kujua hali ya mchezaji huyo baada ya taarifa ya jana kuwa leo ndio yatatoka majibu rasmi kutoka kwa Daktari.
Rweyemamu amesema kuwa Wawa hatokuwa sehemu ya wachezaji watakaosafiri kesho kuelekea Lubumbashi nchini Congo kutokana na majeraha aliyonayo itambidi awe nje ya Uwanja kwa muda wa takribani wiki mbili.
.
‘”Wawa bado ni Majeruhi na hatakuwa sehemu ya wachezaji tutakaosafiri nao hapo kesho kwenda Lubumbashi kwa ajili ya mchezo wetu na TP Mazembe, maana hata mazoezi hajaanza kufanya .
Atakaa nje ya Uwanja kwa takribani wiki mbili ” Rweyemamu