Kane anaweza asicheze tena msimu huu
“Tuna wasiwasi anaweza kukosa kipindi chote cha msimu kilichobaki” Kocha wa Tottenham Hotspur akimuongelea mshambuliaji wake Harry Kane ambaye aliumia katika kifundo chake cha mguu wa kushoto kwenye mchezo wa jana wa robo fainali klabu bingwa Ulaya dhidi ya Man City.
Harry Kane aliumia mwanzoni mwa kipindi cha pili alipokuwa akiwania mpira na beki wa kushoto wa City Fabian Delph.
Kane ameumia katika kifundo kile kile cha mguu ambacho aliumia Januari 13 mwaka huu kwenye mechi dhidi ya Man United ambapo ilipelekea kukaa nje ya uwanja kwa wiki tano.
Mshambuliaji huyo ambaye aliondoka uwanjani na magongo,anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi katika siku chache zijazo ili kujua ukubwa wa tatizo lake.