Rais wa Madrid amkataa Antonio Conte.
Kocha Antonio Conte amejinyima mwenyewe kibarua katika klabu ya Real Madrid baada ya kutaja mahitaji mengi atakapopewa kazi, Raisi wa zamani wa klabu hiyo Ramón Calderón amedai hivyo.
Muitalia huyo alikuwa akihusishwa kuchukua nafasi ya Julen Lopetegui aliyetumiliwa muda kidogo baada ya kupokea kipigo cha 5-1 kutoka kwa mahasimu wao Barcelona.

Kocha wa kikosi B Santiago Solari ndiye amepewa timu kwa sasa wakati wakitafuta mbadala wa kudumu.
‘ Alitaka mkataba wa miaka mitatu na aje na watu watano na awe huru katika kufanya usajili, ‘ Calderon akimuongelea Conte kupitia BBC Radio.
‘ Lakini hicho ni kitu Rais ( Florentino Perez ) hawezi kukubaliana nalo ‘
Calderon ambaye alikuwa Rais wa Real Madrid kwa kipindi cha miaka mitatu, 2006 mpaka 2009 pia alihojiwa kama kocha huyo wa zamani wa Chelsea atakuwa ni chaguo sahihi kwa kazi hiyo ya Real Madrid.
‘ Sifikirii Antonio Conte atakuwa kocha ambaye Bernabeu wanamtarajia. Yupo kama Mourinho – Ni kocha wa kujilinda, kawaida anacheza na mabeki wakati watatu na kushambulia kwa kushitukiza
Hicho si ambacho Real Madrid wanataraji kuona. Rais alijaribu hilo hapo nyuma na Mourinho. Hakushinda kombe la Klabu Bingwa Ulaya, na akaondoka klabuni katika mazingira mabaya ‘
Kocha wa Belgium Roberto Martinez ameibuka kuwa wa mbele zaidi kwa wanaotajwa kuchukua kibarua hicho badala ya Real kulazimishwa kubadili chaguo.