Yanga wasisitiza kuutaka Ubingwa
Baada ya ushindi wa jana wa bao 2-0 dhidi ya Afrika Lyon,Kikosi cha Yanga SC kimeendelea kujifua kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kwaajili ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar.
Mchezo huo utachezwa April 11 mwaka huu ( Alhamis) saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mratibu wa Klabu hiyo Hafidhi Salehe amesema kuwa baada ya kuchukua pointi tatu jana kwa Afrika Lyon watauendeleza moto huo siku ya Alhamisi kwenye mchezo wao na Kagere sugar. ” .
Tunamshukuru Mungu baada ya ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Afrika Lyon kikosi kimeendelea na mazoezi leo asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa Alhamisi na Kagera Sugar, na Mwalimu ameyafanyia kazi mapungufu aliyoyaona kwenye mechi zilizopita na japo mechi itakuwa ngumu lakini tutachukua tena point tatu kwa Kagera Sugar ” amesema Salehe
.
Salehe ameongeza kuwa japo Ligi bado ni ngumu na idadi ya mechi walizopoteza amesema kuwa imani ya kuwa Mabingwa wa Ligi kuu bado ipo na watapambana kuhakikisha wanakuwa Mabingwa. .
.
” Japo tumepoteza michezo kadhaa lakini bado tuna-imani ya kuchukua Ubingwa na ukiangalia katika msimamo wa Ligi kuu bado tunashika nafasi ya kwanza imani yetu bado ipo ya Yanga kuwa Bingwa msimu huu” ameeleza Salehe
.