De Bruyne awashangaa wanaosifia uwanja mpya wa Spurs
Nyota wa Man City Kevin de Bruyne amegoma kufuata upepo wa watu wanaoendelea kusifia uwanja mpya wa Tottenham Hotspur uliozinduliwa wiki iliyopita.
Kuelekea mechi ya robo fainali klabu bingwa Ulaya kesho kati ya Tottenham Hotspur na Man City itakayopigwa katika uwanja mpya wa Spurs,KDB amesema haoni kama ni kitu cha maana watu kuendelea kuusifia uwanja huo na kuamini kuwa utawapa faida zaidi Spurs kwenye mchezo huo.
Tottenham walizindua uwanja wao huo uliowagharimu Pauni Bilioni 1 wiki iliyopita na kesho itakuwa ni mechi yao ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya kucheza kwenye uwanja huo.
.
‘Kila mtu anaongelea uwanja kama kitu fulani cha kipekee.
Kila mmoja ana uwanja.Kila mmoja ana mashabiki’ amesema De Bruyne.
.
‘Mimi sijali kuhusu uwanja, ninajali kuhusu timu tunayocheza nayo. Sifikirii kama kutakuwa na tofauti yoyote.’