Shabiki wa Simba aliyetembea kutoka Mbeya mpaka Dar kupelekwa Lubumbashi
Shabiki wa Klabu ya Simba SC Ramadhan Mohamed aliyetembea kwa miguu kuanzia Machi 26 mwaka huu mpaka April 3 na umbali wa Km 820, kutoka jijini Mbeya mpaka Dar es Salaam kwa miguu ili ashuhudie mchezo wa robo fainali wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe, leo amekutana na viongozi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na sekretarieti ya Klabu hiyo.
.
Shabiki huyo alitumia siku takribani 8 njiani na dhamira yake ya kufika Dar es Salaam ilitimia na moja kati ya Shabiki wa Simba alimkatia tiketi ya laki moja ( platinum tiketi) na kushuhudia mchezo uliochezwa April 6 mwaka huu ambapo katika mchezo huo walitoka Suluhu.
.
Uongozi wa Klabu hiyo umemuahidi shabiki huyo kumgharamia kwenda Lubumbashi nchini Congo kuungana na wanasimba kwenda kuiunga mkono timu yake kwenye mchezo wa marudiano ambao utachezwa Jumamosi Aprili 13, 2019 mwaka huu.
.