Mputu asema kipigo walichokiandaa kwa Simba
Kama kawaida mchezo ukimalizika ni kawaida kwa waandishi wa habari kwenda kupata tathmini ya mchezo kwa kocha, nahodha au mchezaji wowote Yule kutoka pande zote mbili.
Baada ya mchezo wa TP Mazembe na Simba SC kumalizika kwa matokeo ya 0-0 hapoa jana tulimtafuta moja kati ya wachezaji muhimu wa TP Mazembe Tresor Mputu na kumuuliza kuhusiana na tathmini yake katika mchezo ukizingatia ilionekana kama timu yao ilizidiwa na Simba.
Mputu alipoulizwa ili aeleze tofauti ya Simba ya nyuma na sasa alikiri kuwa Simba ni Simba na ni timu nzuri. .
“Kabumbu ndio inakuwaga vile hapa tumeshindwana tunarudi kwetu tutafanya nguvu tuweze kufuzu, Congo hakuna namna itakuwa ni mechi ya nguvu waje tutacheza nao na sisi tutafuzu, Simba ni timu kabambe kabisa ile ya zamani na hii ni Simba tu ni kitu kimoja, sisi tulikuja tupate tatu au tukikosa tatu tupate moja ila wote wachezaji wa Simba wamecheza vizuri” alisema Mputu baada ya mchezo kumalizika