Santiago Bernabeu kuanza kutengenezwa upya
Uongozi wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania umetangaza kuwa utaanza ukarabati wa ujenzi wa uwanja wake Santiago Bernabeu mwishoni mwa msimu huu ukarabati ambao utagharimu takribani miaka mitatu mpaka minne. .
Uwanja huo pamoja na kufanyiwa ukarabati mkubwa ndani ya kipindi cha miaka minne ijayo kuanzia mwisho wa msimu huu, uwezo wake wa kuchukua mashabiki bado utabakia ule ule 81000.
Baadhi ya vitu vitakavyobadilika ni pamoja na mfumo wa ukaaji, na utakuwa na 360 video Screen.
Pamoja na ukarabati huo kuwa na mbwembwe mbalimbali inaelezwa Real Madrid wataendelea kuutumia uwanja huo kama kawaida wakati ukiwa unafanyiwa matengenezo.
Unatazamiwa kuwa ni uwanja wa kisasa wa kufunga na kufungua kwa juu (Open Roof).
Uwanja wa Santiago Bernabeu kwa mara ya kwanza ulijengwa 1944-1947, ujenzi wake uligharimu kipindi cha miaka mitatu.