Bocco ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora
Mshambuliaji wa timu ya Simba SC , John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.
Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Donald Ngoma wa Azam FC na Jaffari Kibaya wa Mtibwa Sugar SC alioingia nao fainali.
Bocco atazawadiwa sh. 1,000,000 (milioni moja) na Tuzo kutoka Biko Sports ambao ndio wadhamini wa Tuzo hizo