Hii ndio sababu ya Rashford kutocheza jana
Mashabiki wa Manchester United mitandaoni wamekuwa wakihoji kukosekana uwanjani kwa mshambuliaji wao Marcus Rashford wakati wa mchezowa ugenini wa Ligi Kuu nchini England dhidi ya Wolves uliyomalizika kwa Manchester United kupokea kipigocha mbao 2-1.
Sababu za kukosekana kwa Rashford katika mchezo huo ni kutokana na kuumwa hivyo kocha mkuu wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer alimuondoa katika orodha ya wachezaji watakaocheza na akiba mapema kabla hata yamchezo na kumuweka Romelu Lukaku kama mbadala wake kutokana na Rashford kuumwa.
Kipigo hicho kimeondoa matumaini ya Manchester United kumaliza nafasi nne za juu katika msimamo waLigi Kuu ya nchini England japokuwa kimahesabu nafasibado wanayo, Manchester United wapo nafasi ya 5 kwasasa wakiwa na alama 61 na wamecheza michezo 32 wamebakisha sita wakati Tottenham nafasi ya nne kwakuwa na alama 61 pia wamezidiwa mchezo mmoja naManchester United.