Ndanda waahidi kifo kwa Yanga Nangwanda
Afisa habari wa klabu ya Ndanda Idrisa Bandari amesema kuwa wana-uhakika wa kumfunga Yanga kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa April 4 mwaka huu (Alhamis) katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza waliocheza Novemba 4 mwaka jana katika Uwanja wa Taifa ambapo Yanga alikuwa mwenyeji Yanga hakuweza kufurukuta kwa Ndanda mpaka dakika 90 zilivyomalizika walitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo huo.
Bandari amesema kuwa mechi zinazochezwa katika Uwanja wao wa Nyumbani wanahakikisha timu yoyote watakayokutana nayo wanapata matokeo mazuri katika Uwanja wao wa Nyumbani.
.
” Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu wa Alhamis maandalizi yamekamilika na kilichobaki ni kumfunga tu Yanga, kama kwenye Uwanja wake wa Nyumbani tuliweza kutoka sare sasa hakuna kingine zaidi ya kumfunga tu” Bandari
Ndanda FC anakutana na Yanga akiwa anashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara na ana point 36 huku Yanga akiwa nafasi ya kwanza kwa kuwa na point 67.