Okwi kujiunga na Simba leo Morogoro
Baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam akitokea katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya nchini Uganda ‘the Crane’s’,Mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC Emmanuel Okwii atajiunga leo na wachezaji wenzie waliopo Morogoro.
Meneja wa Klabu hiyo Patrick Rweyemamu amesema kuwa Okwi tayari yupo jijini Dar es Salaam na leo ataelekea mjini Morogoro kujiunga na wachezaji wenzie walioweka Kambi mjini humo kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa April 3 mwaka huu (jumatano) kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambao Simba SC unautumia kama Uwanja wake wa Nyumbani.
.
“Mchezaji Okwi anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzie leo hapa Morogoro, baada ya kuwasili nchini akitokea Uganda katika majukumu ya timu yake ya Taifa” amesema Rweyemamu