Tarehe ya uchaguzi mkuu wa Yanga yatajwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Ally Mchungahela ametangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga, utakao fanyika Mei 5 mwaka huu.
Mchungahela amesema kuwa Fomu zitaanza kutolewa Kesho Makao Makuu ya Klabu ya Yanga mpaka April 7 mwaka huu.
Pia April 11 mwaka huu mpaka April 13 itakuwa ni kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea na April 14 mwaka huu ni muda wa kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa wagombea.
April 30 mpaka Mei 4 mwaka huu ni Kipindi cha kampeni kwa wagombea na Mei 5 ndio utafanyika Uchaguzi huo.