Lebron James ammwagia sifa Derrick Rose.
Ulikuwa ni usiku mzuri kwa Derrick Rose kuonesha kuwa bado anao uwezo.
MVP wa zamani wa NBA alifunga pointi 50 katika mechi ya jana dhidi ya Utah Jazz ambapo ni pointi nyingi zaidi kuwahi kufunga tangu aanze kucheza NBA.
Hakuonesha kiwango bora pekee, bali pia aliiwezesha Wolves kuibuka na ushindi. Katika ushindi huo wa nyumbani wa 128-125, Rose alipiga mitupio miwili muhimu katika dakika za mwisho na pia alizuia mtupio wa Dante Exum ambao ulikuwa unaenda kusawazisha pointi.
Kilikuwa kiwango bora zaidi ambapo ilipelekea mpaka Rose kushindwa kuzuia machozi yake kutoka baada ya mechi kuisha.
Lebron James ambaye alikuwa Cleveland Cavaliers na Rose msimu uliopita alisifia kiwango alichoonesha jana mchezaji huyo.
Lebron : “ Kijana yoyote ambaye anapitia chochote…anaweza kuangalia kiwango alichoonesha Derrick Rose…Hii ndio maana mchezo wetu ni wa ajabu sana. Hata pale shujaa anapoangushwa chini bado ni shujaa na Derrick Rose ameonesha kuwa bado ni shujaa. “
Kwa ambao hawakuangilia mechi hii jana, wamekosa moja kiwango bora kwenye mchezo katika historia ya NBA miaka ya hivi karibuni. Rose alianza mechi hii kufuatia kocha Tom Thibodeau kuwapumzisha Jimmy Butler na Jeff Teague.
Rose ambaye hakuwahi kufunga pointi 40 tangu achukue tuzo ya mchezaji bora wa NBA msimu wa 2010/11, amepitia matatizo mengi ikiwamo kuwa majeruhi mara kwa mara.
Wakati Butler akitaraji kucheza mechi ijayo dhidi ya Golden State Warriors, Pointi 50 za Rose zitakuwa ni ishara njema ya mambo mazuri kuja.
Kama Wolves wanataka kumuuza Butler kwa wanavyotamani , wanaweza kuegemeza nguvu zao katika ushambuliaji kwa Rose.