Simba watuma salamu kwa Mbao FC
Klabu ya Simba SC kupitia kwa Meneja wake Patrick Rweyemamu amesema kuwa kuelekea mchezo wao wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao FC wanaamini watafanya vizuri katika mchezo huo utakaochezwa Machi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro ambapo Klabu hiyo ndio unautumia kama Uwanja wake wa Nyumbani, baada ya Uwanja wa Taifa kufungwa kupisha maandalizi ya fainali za AFCON U17 ambapo Tanzania ndio mwenyeji wa fainali hizo.
Rweyemamu amesema wanaiheshimu Mbao FC maana imewapa wakati mgumu sana katika msimu uliopita na msimu huu pia.
.
” Tunawaheshimu Mbao FC kwa sababu katika msimu uliopita walitupa changamoto na msimu huu pia katika mchezo wa kwanza hatukupata matokeo mazuri,hivyo tumejipanga vizuri na kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo wetu wa jumapili ” amesema Rweyemamu