Leicester kumkumbuka mmiliki wao kwa staili hio
Oktoba 27,2018 ilikuwa siku ya masikitiko makubwa katika soka hususani kwa mashabiki wa klabu ya Leicester City, kwani iliondokewa na mwenyekiti wao bwana Vichai Srivaddhanaprabha aliyepata ajali muda mchache baada ya kupaa na helicopter yake akitokea King Power Stadium.
Mr Vichai alifariki baada ya helicopter hiyo kuanguka akiwa ametoka kuangalia mchezo wa Leicester City dhidi ya West Ham United uliyokuwa umemamlizika kwa timu hizo kugawana alama moja moja kutokana na kutoka sare ya 1-1.
Weekend hii Leicester City watakuwa wenyeji wa AFC Bournemouth katika uwanja wao wa nyumbani King Power, hivyo Leicester City wameamua kusherehekea Birthday ya mwenyekiti wao ambaye ni marehemu Vichai Srivaddhanaprabha kwa kutangaza kuwa siku hiyo kila shabiki atakayekuwa anaingia uwanjani kutazama mchezo huo atakuwa anapewa bia, maji na cupcake kama sehemu ya kusherehekea Birthday ya Mr Vichai ambaye siku yake ya kuzaliwa ni April 4, na angekuwa hai angetimiza umri wa miaka 61.