Mane amzuia Koulibaly kwenda Man United
Nyota wa kimataifa wa Senegal na klabu ya Liverpool ya nchini England Sadio Mane ameshindwa kuficha hisia zake kwa kuonesha kuwa asingependa kuona mchezaji mwenzake na ndugu yake wa Taifa moja Kalidou Koulibaly anajiunga na klabu ya Manchester United.
Sadio Mane akiwa katika majukumu ya kimataifa na timu yake ya taifa ya Senegal, aliona bango la mashabiki wa Senegal likiwa na picha ya Kalidou Koulibaly likionesha akiwa amevaa jezi ya Manchester United kama ishara ya beki huyo kumuhitaji anende Manchester United.
Koulibaly anayeichezea timu ya taifa ya Senegal na klabu ya Napoli ya Italia amekuwa akihusishwa kwa karibu kuhitajika na Manchester United, hivyo mashabiki hao wa Senegal ambao pia inaonesha wanaishabikia Manchester United waliingia na bango hilo kama kushawishi nyota huyo avutiwe na Manchester United
Ndipo Sadio Mane ambaye ni nahodha wa Senegal alikuwa kama anawafuata huku akicheka na kuonesha ishara ya kutokubaliana na mawazo yao ya kumtaka Koulibaly ajiunge na Manchester United.
Liverpool anayoichezea Sadio Mane ni wapinzani na Manchester United hivyo Mane asingependa kuona wapinzani wao wanapata silaha imara.
.
( 🎥 Orange_Senegal/Twitter)