Viongozi wawili wabwaga manyanga Yanga
Viongozi wa Klabu ya Yanga Samwel Lukumay ambae alikuwa ni Kaimu mwenyekiti wa Klabu hiyo pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika wameamua kujiuzulu katika nafasi zao za uongozi ndani ya Klabu hiyo.
.
Kaimu mwenyekiti wa Klabu hiyo Samwel Lukumay amesema kuwa sababu iliyowafanya wafikie maamuzi hayo wote wawili ni kupisha maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo utakaofanyika mwaka huu.
.
“Sisi kwa pamoja tumeamua kujiuzulu ili kupisha Uchaguzi wa Klabu ,ili kuweza kuchagua viongozi ambapo tutapata Mwenyekiti,makamu pamoja na wajumbe watakaoiongoza Klabu yetu”amesema Lukumay