Unai Emery aliwahi ku-bet timu yake ifungwe.
Kocha wa Arsenal kwa mara ya kwanza amefichua kuwa wakati akiwa mchezaji alikuwa aki-bet dhidi ya timu yake aliyokuwa akiichezea.
Na hii yote aliifanya kwa kuwa na imani ndogo na uwezo wa timu yake na uwezo wake.
Katika kitabu chake cha “ Unai Emery, El Maestro “ anasema kuwa “ Maisha yangu ya uchezaji wa mpira miguu yalikuwa ya maumivu makubwa kuliko furaha. Kwa kiasi fulani, uoga ulikuwa katika akili yangu “
“ Kuwa mfano tu, nilipokuwa mchezaji wa Toledo, marafiki zangu wawili na mimi tulikuwa tuna kawaida ya kufanya ubashiri wa matokeo.
Wikendi moja tulikuwa tunacheza na Elche na niliwabashiria kuwa watashinda mechi kwa sababu walikuwa ni bora na ilikuwa ni mantiki. “
Nikaenda kulipa kwa msichana ambaye alitakiwa kupiga mhuri ‘slip’ yangu.
“ Alikuwa shabiki wa Toledo, akawa ananishangaa na akaniuliza ‘ Unawezaje kuweka Elche washinde ? Unawezaje kufanya hivyo ? ‘
“ Nilijifunza somo kutoka kwake. Ninawezaje kucheza mechi nikiwa na mawazo kuwa tunaenda kupoteza ?
“ Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mchakato wa kubadili fikra zangu “
Mpaka leo, Emery,46, bado anazitumia motisha kutoka kwenye kitabu chake mwenyewe ili kuenda sawa na presha katika kazi yake ufundishaji.
Mchezaji mwenzake wa zamani wa Toledo Alberto Benito aliwahi kusema “ Unai alikuwa winga mwenye kasi, mzuri akiwa na mpira miguuni mwake, lakini kiakili alikuwa anakosa kitu fulani.
“ Punde kukiwa na Presha yoyote, hakuweza kuhimili “