Jose Mourinho amkataa Mbappe
Kocha wa zamani wa timu za Manchester United, Chelsea na Real Madrid Jose Mourinho ambaye anahusishwa kuwa mbioni kuanza kazi ya ukocha kwa mara nyingine tena mwisho wa msimu huu baada ya kufutwa kazi Desemba 2018 Man United ameeleza kuwa kwa sasa kwa upande wake anaamini kuwa mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe ndiye mchezaji ghali zaidi ya wote duniani .
Mourinho alimmwagia sifa mchezaji huyo na kusema kwa sasa hakuna timu yenye uwezo wa kumnunua nyota huyo kutokana na ukubwa wa thamani yake.
.
“Siwezi sema kwa sasa kwamba yeye tu (Mbappe) ndio mchezaji bora duniani lakini kwa maoni yangu ni moja kati ya wachezaji muhimu katika soko kwa sasa, kama ningekuwa kocha katika klabu yoyote kwa sasa nisingemfikiria hata Kyliane Mbappe kwa sababu hanunuliki ila kama kuna mtu anataka kujaribu kila la kheri kwake” alisema Jose Mourinho kupitia Canal Plus
Tukukumbushe tu Kyliane Mbappe aliyetajwa na Jose Mourinho kuwa hanuliliki kwa sasa, alinunuliwa na PSG 2017 akitokea AS Monaco kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 180 na kuwa mchezaji wa kwanza mdogo kununuliwa kwa dau hilo wa pili kwa kununuliwa gharama kubwa duniani baada ya Neymar, katika msimu huu Mbappe kwenye Ligue 1 amefunga mabao 26 katika michezo 23 na ameisaidia Ufaransa kutwaa Kombe la dunia 2018.
Real Madrid ndio timu inayotajwa kuwepo katika mbio za kusaka saini yake.