Ni Arsenal vs Tottenham robo fainali Carabao
Baada ya matokeo ya jana ya ushindi wa goli 2 – 1 dhidi ya Blackpool, klabu ya Arsenal itaikaribisha Tottenham nyumbani kwenye mchezo wa robo fainali. Tottenham wametinga hatua hii baada ya kuichakaza West Ham goli 3 – 1. Mechi hii itachezwa wiki mbili baada ya Arsenal kucheza na Spurs Emirates mchezo wa ligi.
Matokeo mengine ni Middlesbrough wamefanikiwa ingia hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Crytal Palace 1 – 0 na sasa watakutana na Burton Albion walioibuka na ushindi wa goli 3 – 2 dhidi ya Nottingham Forest.
Mechi nyingine zinazotarajiwa kuchezwa ni mabingwa watetezi Manchester City dhidi ya Fulham na mshindi kukutana na mshidni wa mechibya Leicester City dhidi ya Southampton.
Mechi hizi zinatarajiwa chezwa Disemba 17.