Rais Magufuli atoa zawadi ya viwanja kwa Taifa Stars
Rais Magufuli ametoa zawadi ya viwanja kwa kila mchezaji wa Taifa Stars na bondia Hassan Mwakinyo kufuatia kazi nzuri waliyoifanya ya kulipa heshima Taifa la Tanzania.
Pia wachezaji wa zamani wa Taifa Stars Peter Tino na Leodegar Tenga nao wamepewa zawadi ya viwanka
Viwanja hivyo watakavyopewa vipo mkoani Dodoma.
Rais huyo ametoa zawadi hizo leo Ikulu jijini Dar es salaam ambapo alikutana na wachezaji wa Taifa Stars na bondia Mwakinyo kwa ajili ya kuwapa pongezi.
Pia Rais Magufuli ametoa kiasi cha Tsh Bilioni 1 kwa timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON-17 inayotaraji kufanyika nchini Tanzania April mwaka huu.