Jose Mourinho amchana Paul Scholes
Mkongwe wa zamani wa Manchester United Paul Scholes inawezekana akawa ndio kocha aliyeweka rekodi ya kuka muda mchache zaidi katika klabu baada ya kuajiriwa ukizingatia na wengine, Paul Scholes hivi karibu ametangaza kujiuzulu nafasi ya ukocha mkuu wa kuifundisha timu ya Oldham FC ya nchini England kwa madai ya kuingiliwa majukumu yake.
Kilichowashitua wengi ni kutokana na Paul Scholes aliyekuwa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka Sky Sports, kuondoka kwa kujiuzulu katika klabu hiyo akiwa kafanya kazi kwa siku 31 tu na kuachia ngazi, baada ya kuacha kazi hiyo Jose Mourinho ambaye amewahi kukosolewa na Paul Scholes wakati akifanya kazi ya uchambuzi amemkejeli na kumwambia arudi tena studio kuendelea na kazi ya uchambuzi.
“Paul Scholes alikuwa akinikosoa nilipokuwa kocha katika vilabu mbalimbali vikubwa duniani wakati yeye (Scholes) ameweza kuifundisha klabu na kudumu kwa siku 31 tu akiwa na Oldham Athletic, arudi tena studio” alisema Mourinho na kunukuliwa na Bewarmers
Scholes anaachana na Oldham FC kama kocha mkuu akiwa kaifundisha katika michezo 7, akishinda mmoja, sare 3 na amepoteza michezo mitatu, hata hivyo Scholes kabla ya kuanza kazi ya ukocha alikuwa mchambuzi wa soka wa Sky Sports na amewahi kuichezea Manchester United kwa miaka 22 toka enzi za timu za vijana (1991-2013).