Zlatan awapa madongo magwiji wa Man United
Nyota wa zamani wa timu za Manchester United na Paris Saint Germain anayeendesha maisha yake ya soka kwa sasa kwa kuitumikia LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic amewatupia dongo wakongwe wa zamani wa Manchester United kuhusiana na utamaduni wao wa kupenda kuwakosoa wachezaji wa Manchester United hususani Paul Pogba.
Kauli ya Zlatan imewalenga wakongwe wa zamani wa Manchester United ambao walikuwa wakifundishwa na Sir Alex Ferguson wamekuwa wakikosoa sana wachezaji wa sasa, wanasoka waliolengwa na Zlatan ni Class of 92 ambao ni Ryan Giggs, Gary Neville na Paul Scholes kwa sasa wengi wao wanafanya kazi za uchambuzi wa soka.
“Hawachezi tena na wapo kwenye TV na wanalalamika muda wote kwa sababu hawapo tena katika klabu, kama unataka kwenda kufanya kazi katika klabu nenda katafute hiyo kazi katika klabu husika.
“Pogba alikuwa na Manchester United wakati akiwa mdogo, akahama na akarudi tena”
“Katika utawala wa Ferguson, hawakuwa wanapenda hilo kwa sababu walikaa chini ya Ferguson maisha yao yote na hawakuwahi kuhama kutoka kwa Ferguson “
“Hawakuwahi hata kuongea kama Ferguson anakuwa hajawaruhusu kufungua mdomo, hivyo kwa sasa ninavyowaona wanaongea sijui kama Ferguson kawaruhusu au vinginevyo”