Mchezaji wa Marekani aipaisha Tanzania
Futi 19,341 kutoka usawa wa bahari ndio urefu wa mlima mrefu zaidi barani Afrika, mlima huo ambao ni kivutio kikubwa kwa watu mbalimbali duniani unapatikana mkoani Kilimanjaro katika nchi ya Tanzania, unaitwa mlima Kilimanjaro.
Machi 18,mwaka huu nyota wa wa mabingwa wa Super Bowl 2017 Philadelphia Eagles ,Haloti Ngata alikuwa juu ya kilele cha mlima huo akitangaza rasmi kustaafu NFL baada ya kudumu kwa muda wa miaka 13.
Bingwa huyo wa Super Bowl 2012 anastaafu katika ligi hiyo ya American Football akiwa na umri wa miaka 35.
Ngata anakumbukwa kwa umaarufu wake na kupendwa na mashabiki, na siku zote alikuwa mtu mwenye tabasamu pomoni nje ya uwanja na umakini wake mkubwa akiwa ndani ya uwanja.