KDB ajiunga na Jay Z Roc Nation
Nyota wa Man City Kevin De Bruyne amejiunga na kampuni ya usimamizi ya Roc Nation Sports Agency inayomilikiwa na msanii wa Marekani Jay Z.
KDB anaungana na Eric Bailly, Romelu Lukaku na Jerome Boateng wa Bayern Munich ambao nao wapo chini ya usimamizi wa kampuni hiyo.
Roc Nation Sports ni tawi la kampuni ya Roc Nation, kampuni ya burudani iliyoanzishwa na Jay-Z
Tawi hilo la michezo lilianzishwa mwaka 2013 na likiwa na lengo la kusaidia wanamichezo ndani na nje ya uwanja kama vile masuala ya kibiashara, vyombo vya habari na mipango ya kujenga jina ( Brand)