Yussuf Poulsen anataraji kupata mtoto wa kiume
Ni siku nne zimepita tokea mchezaji wa kimataifa wa Denmark mwenye asili ya Tanzania anayeitumikia klabu ya RB Leipzig ya nchini Ujerumani Yussuf Poulsen atangaze kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia RB Leipzig.
Poulsen ameendeleza kutoa habari njema kwa kila mtu anayemfuatilia katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Yussuf Poulsen ametangaza na kuweka bayana kuwa sasa anatarajia kuwa baba wa mtoto wa kiume atakayeitwa Far, hiyo ni kutokana na post yake ya instagram.
Yussuf alitumia ukurasa wake rasmi wa instagram kupost jezi mbili kubwa na ndogo, ndogo ikiwa na jina la Far inayotajwa kuwa ni jina la mwanae anayetarajia kumpata hivi karibuni na jezi ya pili ina jina lake, Picha hiyo ameiambatanisha na maneno yanayoeleza kuwa “Karibuni nakuwa baba” .
Poulsen hajaweka wazi mama wa mtoto huyo ila wadukuzi wa mambo wanafahamu kuwa ni kutoka kwa mpenzi wake wa muda mrefu ambaye amewahi pia kuja nae Tanzania hadi nyumbani kwao Chumbageni Tanga, mpenzi wake anajulikana kwa jina la Maria Duus.
Poulsen ni mdenmark mwenye asili ya Tanzania, mama yake ni raia wa Denmark na baba yake marehemu mzee Yurary alikuwa mtanzania kutokea Tanga