Kante si mtu wa kulewa sifa
Pamoja na kuwa kiungo mkabaji wa Chelsea Ngolo Kante amekuwa na kiwango kizuri katika kazi yake ya soka kwa miaka ya hivi karibuni, kiasi cha kuwa na mchango muhimu katika klabu yake ya Chelsea na timu yake ya taifa ya Ufaransa, kiungo huyo amezidi kuonesha kuwa hajalewa sifa na mafanikio.
Wakati huu wa mapumziko ya Ligi mbalimbali za soka duniani kwa ajili ya kupisha mechi za kimataifa, Ngolo Kante ni sehemu ya wachezaji wa Ufaransa walioitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo na kocha wao Didier Deschamps. Kante ameonesha nidhamu ya hali ya juu ambayo huoneshwa na wachezaji wachache sana.
Kante ameonesha nidhamu ya hali ya juu baada ya kuwasili katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa saa tano na nusu kabla ya muda waliokuwa wamepangiwa kufika, Kante amefika katika kambi hiyo saa 12:30 asubuhi wakati walikuwa wakihitajika kufika saa 6:00, Kante amekuwa na muendelezo wa nidhamu ya hali ya juu iliyopita kiwango kiasi cha kuwa anasifiwa na kila mtu.