Suarez kukaa nje kwa wiki 2
Klabu ya Barcelona leo imetangaza kuwa baada ya vipimo kufanyika, mshambuliaji wao Luis Suarez atakuwa nje ya uwanja kwa siku 10 mpaka 15 kutokana kuumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Real Betis.
Wakati akiendelea kujiuguza mchezaji huyo amejitoa kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa ya Uruguay ambayo inataraji kucheza na Uzbekistan ijumaa hii katika michuano ya China Cup huko nchini China.
Suarez anataraji kuwa fiti kabla ya Barca kushuka dimbani April 10 Old Trafford kucheza mechi yao dhidi ya Man United katika hatua ya robo fainali.