Liverpool wanamuhitaji Ramsey
Ni maneno ya gwiji wa zamani wa Liverpool Steven McMahon alipokuwa katika mdahalo kwenye kituo cha SkySports akiongelea swala la mchezaji huyo wa Arsenal anaetazamiwa kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu klabuni hapo.
Amesema Liverpool watafanya jambo la maana kumchukua kiungo huyu zaidi kwa sababu kuwa hawana mcheza wa aina yake.
“Wana viungo wazuri, washambuliaji wazuri wanaoweza kufunga na hata mabeki wazuri, lakini hawana kiungo wa aina ya Ramsey.”
“Arsenal wapo na kiwango chao cha mishahara, Liverpool hivyo hivyo ila Liverpool wapo na uwezo wa kulipa mshahara wa Ramsey kwa soko la sasa.”
Kuhusu Ramsey kupata namba alisema “Liverpool wamekuwa wakimbadilisha Henderson na Naby Keita hivyo ni mmoja kati ya hawa. Fabinho sio mtu sahihi kwangu.
Kuna kitu kinatakiwa semwa. Ramsey ni bora kuliko Adam Lalana na Xherdan Shaqiri na anaweza kuja na akagombea namba bila wasiwasi.”