Baada ya siku 31, Scholes aachana na Oldam
Mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye kwasasa alikuwa kocha wa klabu ya Oldham Paul Scholes amefikia maamuzi ya kujiuzulu kazi yake hiyo ya ukochakatika timu ya Oldham inayoshiriki Ligi ya Pili England (League Two) kwa sababu za kuingiliwa majukumuyake.
Paul Scholes aliyeripotiwa kujiuzuli nafasi yake yaukocha wa Oldham baada ya kuifundisha timu hiyo kwa siku 31, amefikia maamuzi hayo baada ya kuona mmilikiwa timu ndugu Abdallah Lemsagam ambaye amekuwa akimuangalia katika upangaji wa kikosi cha timu hiyokitu ambacho ameshindwa kukifumbia macho.
Scholes anaachana na Oldham FC kama kocha mkuuakiwa kaifundisha katika michezo 7, akishinda mmoja, sare 3 na amepoteza michezo mitatu.
Scholes kabla ya kuanza kazi ya ukocha alikuwa mchambuzi wasoka wa Sky Sports na amewahi kuichezea Manchester United kwa miaka 22 toka enzi za timu za vijana (1991-2013).