Simba SC ndio habari ya mjini
Historia imeandikwa katika uwanja wa Taifa Dar es salaam jana Machi 16, Simba wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya AS Vita ya Congo.
Magoli ya Mohamed Hussein Tshabalala na lile la ushindi la Clatous Chama dakika ya 90 yamewapelekea Simba hatua hiyo wakishika nafasi ya pili katika kundi D wakiwa na pointi 9, huku Al Ahly wakishika nafasi ya kwana na pointi 10.
Timu zilizofuzu hatua hiyo ya robo Fainali ni Wydad Casablanca,Esperance de Tunis,TP Mazembe, Al Ahly, Simba SC, CS Constatine,Horoya na Mamelod Sundowns.
Droo ya kupanga mechi za robo fainali inataraji kufanyika Jumatano hii Machi 20,2019.