SPURS ITACHEZA NA MANCHESTER CITY MARA TATU NDANI YA SIKU 11
Ratiba ya mechi za robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zimepangwa jana kwa timu zote nane kupata nafasi ya kujua mshindani wake katika hatua hiyo baada ya droo kuchezwa, timu za England Manchester City na Tottenham Hotspurs zimepangwa pamoja.
Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imezipanga Manchester City na Tottenham kucheza hatua ya robo fainali, mchezo wao wa kwanza ukichezwa April 9 2019 Tottenham akiwa mwenyeji na mchezo wao wa marudiano ukichezwa April 17 2019 katika uwanja wa Etihad.
Kutokana na kupangwa ratiba hiyo na timu hizo zinazocheza Ligi moja ya England, watatakiwa kucheza tena mchezo wao wa Ligi Kuu ya England April 20 2019, Machester City wakiwa nyumbani, kutokana na ratiba hiyo sasa ni kwamba timu hizo zitachuana mara tatu ndani ya siku 11 ikiwa ni kuanzia (April 9 2019- April 20 2019)
Kwa upande wa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa timu hizo sasa zimepishana kwa alama 13, Manchester City wakiwa wanaongoza Ligi Kuu England kwa kuwa na jumla ya alama 74 walizopata katika michezo yao 30 wakakti Tottenham wakiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 61 wakiwa wameshacheza michezo 30 hadi sasa.