NYOTA MWENYE ASILI YA KITANZANIA KAZIDI KUAMINIWA BUNDESLIGA
Klabu ya RB Leipzig ya nchini Ujerumani imezidi kuwa na matumaini na imani na mshambuliaji wao wa kimataifa wa Denmark mwenye asili ya Tanzania Yussuf Yurary Poulsen baada ya kuamua kumuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu yao.
Poulsen ambaye amedumu na timu ya RB Leipzig kwa muda mrefu sasa ameongezwa mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia RB Leipzig hadi 2022, Poulsen kwa sasa ana umri wa miaka 24, hadi sasa Poulsen ana mwaka wa sita akiichezea RB Leipzig aliyojiunga nayo 2013 akitokea Lyngby BK ya nchini kwao Denmark.
RB Leipzig inayochezewa na Poulsen aliye na asili ya Tanzania kwa baba akitokea Tanga na mama yake nchini Denmark, timu yake ya RB Leipzig ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchini Ujerumani ikiwa na alama 46 ikicheza michezo 25, wakiwa wamezidiwa na FC Bayern na Dortmund kwa alama 11 ambapo wote wanafanana alama kwa kuwa na alama 57.